HAKOLUBASI AU SAYARI NYEKUNDU
Kitabu kwa ubinadamu
Kitabu bila malipo

Ninachothibitisha kwenye kitabu hiki ni unabii ambao utatimizwa hivi karibuni kwa kuwa nina hakika kuhusu miwaho wa sayari hii; ninajua fika. Sidhamirii kuwatia hofu bali ninawaonya kwa kuwa nimesononeshwa na uduni wa wanadamu. Matukio haya hayatachukua muda mrefu kabla ya kutokea hivyo hakuna muda wa kupoteza kuhusu vitu vya kukisia. - V.M. Rabolu

Katika pande zote za ulimwengu tunapata hadithi za kitamaduni na unabii kuhusiana na nyakati za mwisho, wote huu unafanana na mwingine.

Mwingi wa utabiri huu unatuonya kuhusu majanga makuu katika dunia kama vile kusonga kwa sehemu fulani za ulimwengu, kuyeyuka kwa theluji na kutoweka kwa sehemu kubwa za nchi kutokana na zilizala zenye nguvu na Tsunami.

Kuna unabii usiohesabika umbao una kitu fulani kwa pamoja: unazungumzia hasa kuhusu kukaribia kwa sayari kubwa ambayo huja karibu nasi wakati mwingine. Sayari huenda ilifika kwenye mfumo wetu wa falaki kipindi kilichopita na kuleta maafa yaliyoondoa ustaarab huko Lemuria na Atlantis. Sasa, huenda ikaja kufikisha kikomo ustaarab wetu na hivyo kuwa na kukua kwa awamu mpya.

Inajulikana kwenye tamaduni nyingi, unabii na vitabu vitukufu kwa majina mbalimbali kama vile: Baal, Sayari Baridi, Wormwood, Ajenjo, Hakolubasi, Barnard I, na mengine mengi. Sayari kama hiyo itakuwa tayari inaonekana kwa darubini na ukubwa wake utakuwa mara sita kuliko ule wa Mshtarii.

Katika ujio na kutoka katika maisha, kila kitu hurudi katika mwanzo wake au katika mwisho wake. Kwa hivyo, katika kukutana kulilopita Hakolubasi ilifikisha kikomo ustaarab wa Wanaatlantis. Ukweli huu unahusina kabisa kwenye ‘Mafuriko ya Ulimwengu’ ya dini na mila mbalimbali.

Watu wengi wamezungumza kuhusu matukio ya kilimwengu. Mmojawapo alikuwa V.M. Rabolu, ambaye alidadisi kuhusu karibia kwa sayari hiyo kwa kutumia kigezo cha fahamu wazi, ambazo zilimwezesha kutafiti kuhusu umbo hili la mbinguni. Katika kazi yake yenye Kichwa ‘Hakolubasi au Sayari Nyekundu’, ambayo hutumwa bila malipo ulimwenguni kote na Shirika la Alcione, anaandika:

‘Wakati Hakolubasi inakuja karibu na Dunia na kuwa sambamba na Jua, majanga mabaya yataanza kuenea kote katika sayari yote. Si madaktari wala sayansi rasmi itakayojua ni aina gani ya maradhi au jinsi ya kuyatibu. Watakuwa hawana nguvu mbele ya majanga haya.’

‘Wakati janga na giza litakuja: mitetemeko ya ardhi, zilizala na mawimbi makali. Wanadamu watakuwa wamepoteza urazini, kwa kuwa hawataweza kula au kulala. Mbele ya hatari, watajitupa kwenye hatari ya halaiki na kuwa wehu kabisa.’

V.M. Rabolu

V.M. Rabolu, mtafiti mkuu wa Kolombia katika unajimu, aliinua sauti yake kuwaonya wanadamu kuhusu tishio hili. Anasema wazi, ukweli kwamba, linaweza kufikisha kikomo utaarabu wetu na utamaduni wetu. Katika kitabu chake, anafundisha mbinu ya kuondoa ulemavu wa kisaikolojia na njia za kuangaziwa kwa kinajimu kuwa mbinu za pekee zilizopo kuliepuka janga linalokuja.

V.M. Rabolu anamalizia kazi yake kwa kusema: ‘Msomaji mpendwa: ninaongea kwa wazi kabisa ili uelewe haja ya kufanya bila mzaha. Yeyote anayefanya ataokolewa kutoka kwenye janga. Huku si kuja na nadharia au kuwa na kuchangizana bali kuwa na ujuzi wa mafunzo ya ukweli ambayo ninawapa kwenye kitabu hiki. Tusiendee chochote zaidi.’

Shirika la Alcione

Shirika lisilolenga kutafuta faida liliteuliwa kuwa wakala mshirika katika kueneza na kusambaza kazi ya ‘Hakolubasi au Sayari Nyekundu’

Mwandishi: Joaquin Amortegui Valbuena (V.M. Rabolu)
Matibaa: Angel Prats

Shirika la Alcione limesajiliwa na Sajili ya Taifa ya Mashirika katika Wizara ya Masuala ya Ndani, Kikundi 1, ibara 1, na nambari ya taifa 588698, na lina makao yake makuu huko P.O. Box 4, 09080, katika mji wa Burgos (Uhispania).

Kuhusu mwandishi

V.M. Rabolu (1926-2000)
V.M. Rabolu (1926-2000)

V.M. Rabolu (1926-2000) alizaliwa huko Tolima (Kolombia). Mwaka wa 1952 alipata Ufahamu wa kweli na kupitia mwaka mingi wa majaribio ya kinajimu alikuwa fahamu za ajabu ambazo baadaye zilimbadilisha kuwa mwelekezaji wa kiroho ambaye alijulikana ulimwenguni kote.

Akiwa na welewa kuwa siku za usoni zinatusubiri, alijitolea kuwafundisha wanadamu mbinu za kutimiza ukuzaji wao wenyewe wa kiroho. Kwa hivyo, kuanzia miaka ya 70 na wakati wote kwa kufurahisha wengine na kutokuwa na ubinafsi alianza jukumu la kuchosha hadharani hekima ya kweli kwa maongezi, vipindi na makongamano katika ngazi ya kimataifa.

Mnamo mwaka wa 1988 aliandika “Hercolubus au Sayari Nyekundu” akijikita kwenye fahamu zake na tajriba pana, V.M. Rabolu anaelezea matukio ya kutisha ambayo yatafanyika katika sayari yetu kwa njia fupi and kutoa maelezo kuhusu njia wanadamu wanaweza kufuata ili kuafikika kubadilika kwa ndani. Siku hizi, kauli zilizomo kwenye kazi yake zinatambuliwa na idadi kubwa ya wasomaji ambao wamefaidika kutokana na mafunzo yake katika zaidi ya mataifa 60.

V.M. Rabolu alikuwa mmoja wa wale watu adimu wenye Fahamu Tambuzi. Mafunzo yake ni muhimu katika nyakati hizi ambapo kupenda mali na ukosefu wa maadili umekuwa ishara wazi za jamii ambayo imepotea zaidi.

“Mimi zi mwenezaji wa umbeya; mimi ni wanadamu ambaye ninaonya kuhusu kile kinaenda kufanyika”

V.M. Rabolu

Vibwagizo

Katika kipengele hiki, unaweza ukamsikiliza V.M. Rabolu akitamka vibwagizo kwa ajili ya kuangaziwa kwa kinajimu, ili ufahamu kutamka kunakofaa.

FA RA ON

LA RA S

Shirikiana na Shirika la Alcione

Shirika la Alcione ni shirika ambalo limesajiliwa kisheria. Kama shirikia lisilotafuta faida, shughuli zake zote zinafanywa kwa ajili ya furaha za wengine bila haja yoyote ya kupata fedha.

Shirika la Alcione liko kama wakala mshirikishi wa Bwana Angel Prats, mchapishaji wa kitabu ‘Hakolubasi au Sayari Nyekundu’; kwa hivyo nia yake ya pekee ni uenezaji na usambazaji wa kitabu hicho. Kwa sababu hii, kazi kuu ya Shirika la Alcione inahusisha kutuma nakala bila malipo katika sehemu yoyote ulimwenguni katika jaribio la kueneza kazi hiyo na ujumbe wake wa ulimwengu kwa mtu yeyote aliye na ari bila kutofautisha.

Hadi sasa, kampeni ya usambazaji imewezesha maelfu ya wasomaji kupokea kwa njia ya barua pepe nakala bila malipo ya kitabu ‘Hakolubasi au Sayari Nyekundu’. Kwa sasa na siku baada ya siku idadi ya maombi inaendelea kuongezeka. Kwa ajili ya ufanisi huu mkubwa, tumejiwekea nia ya kuendelwa na kampeni hii ya usambazaji.

Tafadhali tusaidie katika uenezaji wa kazi hii kwa kupata Video na kuituma kwa njia ya barua pepe kwa marafiki na wahisani.

Ikiwa ungependa kuwasiliana na Shirika letu au kama una ari ya kushirikiana nasi kuhusiana na usambasaji wa kitabu cha V.M. Rabolu na ujumbe, au ikiwa unahitaji kuwa na mawasiliano thabiti na kujiunga nasi, unaweza kuandika kupitia kwa anwani zifuatazo:

Barua pepe kwa: [email protected]

Kwa anwani ya kawaida:
Asociación Alcione
P.O. Box 4, 09080 Burgos (Spain)

Omba kitabu chako bila malipo

Kitabu hiki Kimetafsiriwa kwa lugha kadhaa na kimesambazwa katika zaidi ya nchi sitini.

Fomu ya kuagizia

Data ambayo imewekewa alawa ya kinyota (*) ni muhimu katika kuongoza agizo. Ujumbe huu umekusanywa na unatumiwa kwa njia ya pekee kuafikia vigezo vya kuagizia kitabu.

Ili kupokea kitabu, lazima utumie anwani sahihi ya barua pepe.

Kukamilisha ombi lako, soma na uhakiki kisanduku hiki.

Kwa kubonyeza kwenye kidude cha kuwasilisha, unakubalikiana na mchakato wa kupata data kwa maagizo ya, na kwa taratibu zilizowekwa, Sera ya Siri.

Alcyone Association